14 Juni 2013 - 19:30
Iran yapata rais mpya

Baada ya kufanyika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran ambao ulifanywa na wananchi waliopo Iran na waliopo nje ya Iran. hatimaye Hassan Rohani amechukua nafasi ya kiti cha uraisi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran.

waziri wa mambo ya ndani ya Iran Mustafa Muhammad Najjar amemtangaza Hassan Rohani kuwa rais mpya wa Iran atakaye chukua nafasi ya Dokta Mahmuud Ahmad Nejad.Hassan Rohani ameshinda kwa kupata kura 18,613,329 sana na asilimia 50.70 ya kura zote.Inafaa kuashiria kwamba uchaguzi huu wa urais ulihudhuriwa na wapiga kura wengi sana ambapo fauka ya asilimia 72 ya waliokuwa na haki ya kupiga kura walishiriki katika zoezi la uchaguzi.